Kutana na wateule wapya katika baraza la mawaziri lake Uhuru Kenyatta

- Uhuru alikamilisha kutangaza baraza lake la mawaziri siku ya jana, Ijumaa, Januari 26

- Katika baraza lake jipya, ni mawaziri 10 waliosalia huku wengine tisa wakitemwa

- Kuna baadhi ya wale walijiunga na baraza hilo la mawaziri chini ya uongozi wa Uhuru kwa mara ya kwanza

Rais Uhuru Kenyatta alikamilisha kulitaja baraza lake la mawaziri baada ya hapo awali kudokeza kuwa kuna wale watakaosalia katika baraza lake, waliohudumu katika muhula wake wa kwanza.

Habari Nyingine: Dada wawili mapacha wafanya harusi ya kifahari Lagos (picha)

Hapo Ijumaa, Januari 26, Uhuru alisema kuwa kuna wale wapya watakaojiunga na baraza hilo, baadhi ya baraza la hapo awali wakisalia huku wengi wakitemwa na kufanya mabalozi.

Hawa ndio waliojiunga na baraza hilo kwa mara ya kwanza kama wateule;

1. Ukur Yatani waziri wa Leba

Alikuwa gavana wa kaunti ya Marsabit.

2. Peter Munya waziri katika jumuiya ya Afrika Mashiriki

Alikuwa gavana wa kaunti ya Meru.

3. Farida Karoney waziri wa Ardhi

Alkuwa mwanahabari na meneja katika shirika la habari la Royal Media Services

4. Rashid Achesa waziri wa Michezo

Alikuwa kiongozi wa vijana wa ODM Magharibi mwa Kenya

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

5. Keriako Tobiko waziri wa Mazingira

Habari nyingine: Mpango wa kando wake Diamond kutoka Rwanda aonekana akiwa na viatu vya bei ghali

Alikuwa mkurugenzi wa mashataka ya umma.

6. Simon Chelgui waziri wa Maji na unyunyiziaji

Alipoteza katika kinyang'anyiro cha ugavana Baringo.

7. Monica Juma waziri wa Mambo ya Kigeni

Habari Nyingine: Hii ndio sababu Rais Yoweri Museveni hujanywa soda tangu 1965

Alikuwa katibu mkuu katika wizara ya Mambo ya Kigeni.

8. John Munyes waziri wa Petroli na Uchimbaji Madini

Alikuwa seneta wa Turkana aliyeangushwa na Josephat Nanok wa ODM katikakinyang'anyiro cha ugavana.

9. Raphael Tuju

Habari Nyingine:

Alikuwa katibu mkuu wa chama cha Jubilee kinachoongozwa na Uhuru. Alichaguliwa bila kuwepo kwa wizara yoyote anayoshikilia.

10. Margaret Kobia waziriwa vijana na utumishi wa umma.

PICHA ZOTE: Hisani

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una taarifa ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Wafuasi wa NASA wahimizwa kususia bidhaa za kampuni ya Haco Tiger – Kwenye TUKO

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4F0go9moq6skaOubrrAZq6arJWquaZ51pqnspldoK61tcqaZJuZopbHonnLmmSmmaeWx6q%2ByGajmqOVYsKpwdGuZKSdnq6utcDAZ5%2BtpZw%3D