Mkuu wa zamani wa posta Francis Chahonyo afariki
-Chahonyo alifariki katika hospitali ya Karen, Nairobi alikokuwa akipokea matibabu
-Aliripotiwa kutibiwa kwa muda mrefu ikiwemo kusafiri kwenda India
-Hata hivyo, familia yake haikufichua alichokuwa akiugua
Mkuu wa zamani wa posta Francis Chahonyo amefariki.
Chahonyo aliyeripotiwa kutibiwa kwa muda mrefu alifariki Jumatatu, Juni 25 katika hospitali ya Karen, Nairobi alikokuwa akitibiwa.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: Raila awaeleze Wakenya alivyojenga nyumba ya KSh 1 bilioni jijini Kisumu – Waziri Achesa

Habari Nyingine: Mume wangu analala na yaya wangu na ninataka kumwadhibu – Mwanamke afichua
Ripoti zilizoifikia TUKO.co.ke zilisema kuwa Chahonyo alilazwa hospitalini miezi miwili iliyopita.
Akidhibitisha kifo chake, msemaji wa familia yake Dan Chitwa alisema Mzee Chahonyo alisafiri nchini India kwa matibabu zaidi lakini hali yake ya afya haikuimarika.
Habari Nyingine: Wakenya wamshauri Uhuru kuhusu vita dhidi ya ufisadi
Kando na kuhudumu kama mkuu wa posta nchini, Chahonyo alifanya kazi kwenye bodi ya kitaifa ya sukari na aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya soka ya AFC Leopards.
Chahonyo anatokea eneo la Chavakali, kaunti ya Vihiga.
Habari Nyingine: Viongozi wa Mlima Kenya wamtaka Kindiki kuwa naibu wa Ruto 2022
Wakati akihudumu kama mkuu wa Posta, Chahonyo alitajwa kwenye sakata tofauti za ufisadi ikiwemo sakata maarufu ya Ango Leasing.
Afisa huyo aliwahi kushtakiwa kwa utumiaji mbaya wa mamlaka lakini akaondolewa mashtaka hayo.
Read ENGLISH VERSION
Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News
Safari ya mwisho ya Kenneth Matiba mjini Murang’a | TUKO TV
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibIR5fpVmpKStpWLEonnZmqSapplixKJ5z6iqrZldm7%2BiusKiqmabmJa1sLrYqGSanpGntqy1jaGrpqQ%3D